SHARE

Mkufunzi wa timu ya taifa Ufaransa Didier Deschamps ameachwa akiwa na ”ghadhabu” baada ya timu yake kushindwa kuifunga Luxembourg licha ya kupata nafasi nyingi, matokeo yaliyotajwa kuwa ya ”kihistoria” na mwenzake wa Luxembourg.

Mechi hiyo iliyochezwa Ufaransa ilimalizika kwa sare tasa.

Ufaransa ilimiliki mpira katika mchezo huo kwa asilimia 76, na kushambulia mara 34 na kugonga mlingoti wa goli mara mbili lakini hawakufanikiwa kuwafunga Luxembourg kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1914.

”Inaghadhabisha kupata nafasi nyingi hivyo bila kupata goli lolote,” alisema Deschamps.

Kocha wa Luxembourg, Luc Holtz amesema: ”Ni siku ya sherehe kwa soka ya Luxembourg”

Licha ya kucheza na timu iliyoorodheshwa katika nafasi ya 136 ulimwenguni, Deschamps aliwasilisha kikosi kilichojaa wachezaji nyota mechi hiyo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia iliyochezewa Toulouse.

Kikosi cha Ufaransa kilikuwa na kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba na washambuliaji Antoine Griezman wa Atletico Madrid na Kylian Mbappe ambaye amejiunga na PSG hivi majuzi kwa mkopo kutoka Monaco ambapo anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa £166m msimu ujao

Griezmann alipiga kiki kutoka ya umbali wa yadi 30 dakika tano kabla ya wakati wa mapumziko huku Pogba akipata mpira wa mrejesho lakini hakuona lango.

Ingekuwa hatari zaidi kwa Les Bleus, mchezaji wa Luxembourg Gerson Rodrigues alipomzidi Laurent Kosscielny dakika ya 79, lakini kombora lake liligonga mlingoti.

Ufaransa, iliyowachapa Uholanzi 4-0 siku ya Alhamisi, wamesalia kileleni mwa kundi A baada ya sare hiyo, lakini uongozi wao umepunguzwa hadi alama moja na Sweden.

”Matokeo ya Alhamisi yalikuwa na umuhimu, na tulihitaji kupata alama tatu tulipokuwa tukikabiliana na Luxembourg, kwa hivyo tunastahili kujikaza hadi mwisho ,”Deschamps aliambia TF1.”

”Michezo miwili ya mwisho, itakuwa yenye uamuzi, tuko katika nafasi nzuri kuliko tulivyokuwa mwezi Juni, licha ya kwamba tumekasirishwa usiku wa leo”.

Luxembourg iliichapa Belarus 1-0 siku ya Alhamisi ukiwa ni mchezo wao wa kipekee waliopata ushindi.

”Tumetosheka na alama hiyo moja, tuliyoipata kwa kucheza na mioyo yetu, jitihada na mafanikio,” aliongeza Holtz.

”Na iwapo tungekuwa na bahati zaidi kungepata alama tatu.

Kwa Luxembourg, matokeo yao ni ya kihistoria. alama moja dhidi ya timu kubwa huwa nadra sana.”


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here