SHARE

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kuwa hayuko tayari kushiriki marudio ya uchaguzi Mkuu wa Urais nchini humo endapo hayatafanyika mabadiliko kwenye Tume ya Uchaguzi nchini humo (IEBC).

Odinga amesisitiza kuwa anataka kuwepo kwa mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika, kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 17 mwaka huu.

Odinga amependekeza kubadilishwa kwa uongozi wa IEBC, ambayo imelaumiwa na mahakama ya juu kwa kuendesha uchaguzi kwa njia ambayo haiukuwa ya haki na kufanya Mahakama hiyo kufuta matokeo ya uchaguzi yaliotangazwa na tume.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here