SHARE

Winga wa timu ya Taifa, Tanzania, Simon Msuva kwa mara ya kwanza atacheza Ligi Kuu ya nchini Morocco akiwa na klabu yake mpya ya, Difaa El Jadida

Ligi Kuu ya nchini Morocco maarufu kama Botola Pro, ilifunguliwa rasmi jana Ijumaa Septemba 8, kwa kupigwa michezo miwili kati ya Racing de Casablanca na KACM, FAR Rabat na Rapide Club Oued Zem.

Difaa El Jadida watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Stade Ben Ahmed El Abdi kuwakaribisha klabu ya Chabab Atlas Khenifra, saa tatu usiku majira ya Afrika Mashariki.

 Difaa El Jadidi imemaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi msimu uliopita ikiwa na pointi 59 nyuma ya WCA Casablanca waliomaliza katika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 66. Ligi kuu ya Morocco inajumuisha timu 16.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here