SHARE

Mshambuliaji chipukizi wa Tanzania, Yohana Oscar Nkomola amefuzu majaribio katika klabu ya Esperance ya Tunisia na sasa anatarajiwa kusaini mkataba.

Akizungumza mjini Dar es Salaam jana baada ya kuwasili kutoka Tunisia, kufuatia majaribio ya wiki tatu, Nkomola amesema kwamba anamshukuru Mungu kwa mafanikio hayo, kwani hizo ndizo ndoto zake.

“Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata nafasi hii na ninaamini huu ni mwanzo mzuri kwangu kuelekea kutimiza ndoto zangu za kuwa mchezaji mkubwa,”amesema.

“Nimerudi hapa nyumbani kukamilisha taratibu fulani, baada ya wiki mbili nitaondoka kurejea Tunisia ambako nikifika kwanza nitaanza kuchezea timu B ya vijana hadi nifikishe umri wa miaka 18 mwezi wa nne (2018) ndipo nisaini mkataba na kuanza kuchezea timu ya wakubwa,”amesema.

Nkomola alikwenda Tunisia pamoja na wachezaji wengine wawili aliokuwa nao timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki Fainali za Vijana Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon, Ally Ng’anzi na Eric Nkosi.
Bahati mbaya kwa Ng’anzi na Nkosi hawakufuzu majaribio na wanarejea nyumbani kuendelea na harakati za kujiinua kisoka.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here