SHARE

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema atakapostaafu kucheza soka anataka kusomea ukocha ili kuja kuchukua mikoba ya kocha wake wa sasa George Lwandamina.

Cannavaro licha ya kuwa na cheo hicho lakini amekuwa hapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza kutokana na umri wake kumtupa mkono.

“Hata kama sichezi lakini nafurahi kuwa benchi kwasababu najifunza mambo mengi kutoka kwa makocha waliopo na lengo langu baada ya kustaafu kucheza nataka kuja kuifundisha Yanga siku zijazo,” amesema Cannavaro.

Nahodha huyo amesema hakuna kinachoshindikana katika hilo kwani kwa kipindi cha misimu 11, alichoitumikia Yanga ameweza kujifundisha mambo mengi kutoka kwa makocha mbalimbali ambao wamepitia timu hiyo.

Mkongwe huyo amesema mipango yake baada ya kustaafu kucheza soka ni kwenda kusomea ukocha ili kuongeza elimu ambayo itamfanya kuwa na vigezo vya kuweza kufundisha timu za Ligi Kuu hasa Yanga.

Cannavaro alijiunga na Yanga mwaka 1997, akitokea Tembo ya Zanzibar akiwa na wenzake watatu ambao ni kipa Mbarouk Selemani, Mohamed Mkweche na Thomas Morice.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here