SHARE

Kocha Msaidizi wa Simba Jackson Mayanja, amesema  sare waliyoipata jana dhidi ya Azam FC,  haikutokana na kumkosa mshambuliaji wao Emmanueli Okwi, ambaye amechelewa kurudi nchini kutoka Uganda alipokwenda kuichezea timu yake ya taifa Uganda ‘The Cranace’.

Mayanja amesema ,wachezaji woo wote walicheza vizuri na kuipigania timu yao lakini wapinzani wao Azam walikuwa imara na kuokoa mashambulizi yote lango ni mwao.

“Sababu ya kukosa ushindi siyo Okwi, bali ni ushindani uliokuwepo kwenye mchezo huo ingawa katika kipindi cha kwanza tungeweza kupata mabao lakini hatukuweza kuzitumia nafasi ambazo tulizipata kipindi cha kwanza,”amesema Mayanja.

 Kocha huyo amesema sare hiyo imewapotezea malengo yao lakini wanakwenda kujipanga ili kuhakikisha wanashinda mchezo unaofuata ambao watacheza nyumbani.

Mayanja amesema mipango yao ni kufanya mazoezi ya nguvu ili kurekebisha matokeo hayo na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo kama ambavyo wamekusudia kufanya wakati ligi inakaribia kuanza.

Sare hiyo dhidi ya Azam FC imeifanya Simba kufikisha pointi nne katika mechi mbili walizocheza na kuendelea kuongoza ligi kwa faida ya mabao mengi ya kufunga katika mchezo wa kwanza walipocheza na Ruvu Shooting ya Pwani.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here