SHARE

Legendari wa Ufaransa Thierry Henry amesema Paris Saint-Germain ni lazima ionyeshe ushindani kwenye Ligi ya Mabingwa kufuatia safu thabiti ya mashambulizi.

Kijana mpya Kylian Mbappe amekuwa mchezaji mwingine mwenye thamani kubwa kufunga kwenye mechi yake ya kwanza baada ya kuungana na Neymar na Edinson Cavani wakitikisa nyavu katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Metz Ijumaa.

Kikosi cha Unai Emery ndiyo timu pekee iliyojiwekea rekodi nzuri baada ya mechi tano za Ligue 1 wanapotaka kuivua ubingwa Monaco.

 Lakini Henry amesisitiza kuwa thamani ya klabu hiyo ni kubwa hasa kufuatia usajili wa Neymar, na hilo litaamua kiwango chao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Neymar na Mbappe wamejiunga na PSG, ni jambo jema sana kwa ligi ya Ufaransa. Itakuza wasifu kwa kiasi kikubwa,” Henry aliandika kwenye gazeti la The Sun.

“Kama ningeambiwa jambo hili lingetokea mwanzoni mwa msimu wa majira ya joto, ningesema, ‘umechanganyikiwa nini?’ ni ajabu sana.

“Kutakuwa na presha kubwa, kwa sababu wameingia kwenye ushindani wa timu zenye majina makubwa.

“Hilo ndilo tunalotarajia kutoka kwa timu kubwa.”

Henry alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa Barcelona 2008-09 baada ya kupoteza fainali akiwa na Arsenal miaka mitatu kabla.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia anaamini ni wakati sahihi kwa timu za Ligi Kuu Uingereza kuleta ushindani dhidi ya utawala wa sasa wa Real Madrid.

“Ni miaka mingi tangu klabu za Uingereza zilipotisha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa,” aliandika.

“Man City wapo vizuri sana, Man United pia. Naam, Spurs huenda wasiwe thabiti sana.

“Lakini kuna timu tano za Uingereza awamu hii, kwa hiyo itakuwa vema kuona moja ikitinga fainali.”


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here