SHARE
Juventus' forward Paulo Dybala from Argentina scores during the Italian Serie A football match Juventus Vs Hellas Verona on January 6, 2016 at the "Juventus Stadium" in Turin. AFP PHOTO / MARCO BERTORELLO / AFP / MARCO BERTORELLO (Photo credit should read MARCO BERTORELLO/AFP/Getty Images)

Wakala Mino Raiola amewaumiza mashabiki wa Juventus kwa kudai kuwa Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala anahitaji kuwahama mabingwa hao wa Italia.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Juve akitokea Palermo mnamo Juni 2015 na amekuwa chachu ya mafanikio ya Binaconeri katika kutetea taji la Serie A msimu uliopita.

Lakini wakala huyo anaamini mchezaji huyo atakuwa na mafanikio zaidi akiondoka Turin – na si lazima atue Barcelona.

 “Nadhani Dybala hatimaye ataondoka Juve,” Raiola alikiambia RaiSport.

“Anahitaji kwenda kwenye timu ambapo atapata kila kitu kipo tayari kwa ajili yake.

“Kwa yeye ni vigumu kujiunga na Barcelona mpya, lakini atafanya vizuri kwa Real Madrid, Manchester United, Manchester City au Chelsea.”

Raiola pia alizungumza kinyume na Mkurugenzi mtendaji wa AC Milan Marco Fassone na mkurugenzi wa michezo Massimiliano Mirabelli, akisema, “Siamini mipango yao ya kazi”.

Fassone amesema Raiola ndiye aliyechelewesha Gianluigi Donnarumma, 18, kusaini mkataba mpya klabuni hapo Julai.

Muitaliano Donnarumma hatimaye alisaini mkataba mpya San Siro, lakini Raiola aliamua kuchukua fursa kuanika hisia zake juu ya vigogo hao wa Milan, ambao wamekuwa kwenye wakati mgumu baada ya kipigo cha 4-1 kutoka kwa Lazio Serie A.

“Sina tatizo lolote binafsi dhidi yao, lakini tatizo ni kwamba sina imani na mipango yao,” Raiola alisema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here