SHARE

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amemwagia sifa mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe, akidai kuwa Mfaransa huyo anaweza kuwa “Pele mpya”.

Arsenal walikuwa miongoni mwa klabu nyingi zilizokuwa zikitaka saini ya Mbappe majira ya joto baada ya mchezaji huyo kuwika akiwa na Monaco iliyotwaa taji la Ligue 1.

PSG wameshinda mbio za saini ya mchezaji huyo kwa dau nono la fedha, na baada ya nyota huyo kinda kufunga katika mechi yake ya kwanza klabuni hapo, Wenger hakuona sababu ya kutomsifia.

 “Nadhani ni mchezaji mwenye akili ya kipekee, anatabia ya kipekee na imani ya kipekee,” Wenger alikiambia BeIN Sports.

“Nawaambia rafiki zangu, ‘Mbappe ndiye Pele mpya’. Anaweza kuwa mchezaji bora duniani, kwa sababu ana haiba, tabia njema na imani njema.

“Huwezi kudhani unazungumza na mtu wa miaka 18 unapoongea naye. Daima huonyesha uwezo mkubwa anapokuwa na mpira na jambo lolote linaweza kutokea.”

Mbappe amefunga mabao 26 katika mechi 44 akiwa Monaco msimu uliopita, na hivi sasa amefungua akunti yake ya mabao Ufaransa pia.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here