SHARE

Umoja wa Vyama visivyokua na wawakilishi bungeni, vimekosoa vikali hatua ya  msajili wa vyama vya siasa hapa nchini Jaji Francis Mutungi kwa kitendo cha  kuwapelekea barua yakuwataka kutoa maoni ya mabadiliko ya sheria ndani ya siku 14 huku ikiwa tofauti na vyama vingine vyenye wawakilishi bungeni vya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR na ACT ambavyo vimepelekewa rasimu ya sheria ya mabadiliko ya vyama vya siasa.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huo bwana Renatus Muhabhi amesema kuwa hawapingani na mabadiliko  hayo lakini  msajili amekua hatendi haki kwa vyama  hivyo 13 ambavyo havina wawakilishi bungeni.

Hivyo ameomba wapatiwe rasimu ya mabadiliko ya sheria mpya ya vyama vya siasa ili waijadili na waweze kutoa maoni yao vizuri na muda uongezwe.

Aliongeza kwa kusema kuwa “tumepokea barua ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria za vyama lakini kwanini upande mwingine wamepewa na rasimu?, kwani kuna utofauti wa chama kimoja na kingine?” Hivyo tunamtaka msajili apitie tena marejeo ya mapendezo yetu ili sisi tuwe sawa na vyama vingine kwani tuna haki Kama vyama vingine.

Hivyo kama kutakua na utofauti wa vyama tunaiomba serikali wafute ruzuku zinazotolewa kwa vyama ili kuondoa utata uliopo kwani vyama hivi 13  havina fedha vinaishi kwa michango na kuombaomba hivyo hutuwezi ndani ya siku 14 kuwa tumewafikia wanachama wetu. Alisema mmoja wa wajumbe wa umoja huo ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha ADC Doyo Hassan Doyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha NRA Hassan Almas ameeleza kuwa kila sheria inataratibu zake, ni vyema msajili akawashirikisha kuliko kuwabagua na kuwapa huo mswada ili waujadili na aongoze muda kutokana na sababu za kiuchumi ndani ya vyama hivyo kwani itawalazimu kuitisha mkutano mkuu kuwajulisha wanachama wao.

Umoja huo umemuandikia barua msajili wa vyama vya siasa siku ya leo na kutoa nakala ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Vyama vya Siasa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here