SHARE

  SEHEMU YA 69

Kipindi wale wachawi wanapanga kuondoa uhai wa mdogo wangu, mdogo wangu alilia sana pale hospitali, maana alikuwa anasikia uchungu usio elezeka masikini, kitendo kilicho wakwaza wengi, sanasana wale waliokuwa wakimfahamu,  wataalamu wote waliosoma udakitari na mdogo wangu walijaribu sana kufanya utafiti wote kwa uwezo na juhudi zao zote ili waweze kunusuru maisha ya rafiki yao lakini hawakufanikiwa, kipindi zimebaki kama dakika 30 ili mdogo wangu apoteze maisha yake ! Nilianza kulia sana mimi pamoja na baba, maana povu lilikuwa limeanza kumtoka mdomoni mdogo wangu, chakula alikuwa hali tena zaidi ya kulishwa na mlija kupitia puani mwake.

Dakitari mmoja akasema “jamani ndugu zangu tumejaribu kufanya kila mbinu ila tumeshindwa maana tumboni kwake tunaona jiwe sio mtoto tena na tunaogopa kumfanyia upasuaji maana damu inamtoka sana sehemu zake za siri hivyo anaweza kufa mda sio mlefu hapa, bora tuwaachie wataaramu wa kimila hii kazi” dooh nikamuuliza “sasa dokta jamani tunamsaidiaje mdogo wangu, ebu tazama macho yake hayaoni sasa, wala hawezi tena kutoa sauti katika kinywa chake”  daktari akasema “nilikuwa namaanisha tumkimbize haraka kwa mganga wa Jadi   mmoja hivi labda anaweza kumsaidia” baba yangu mzazi akakataa akasema “hapana tumuamini mungu tu kwa hili jambo! kwa mganga tusiende, mungu atatusaidia mpaka atapona” na mda huo zimebaki dakika 20 tu kaka yake na mama wa kambo waweze kufurahia kunywa damu na nyama ya mdogo wangu.

Walitaka kumuua ili mambo yote ya mama wa kambo yafanikiwe! asiweze kuteswa kamwe na mizimu na asiteseka kamwe maisha yake yote, Wakati wale madaktari na baba wanabishana kuhusu mganga, ilibidi mdogo wangu abebwe kwanguvu ili akafanyiwe tambiko kwa mganga wa jadi, mdogo wangu akapandishwa kwenye gari akiwa hajitambui na akiwa kakodoa macho sana,  alipo wekwa kwenye gari ili apelekwe kwa mganga. Wale wachawi wakagundua ule mpango ndipo wakaja kichawi kuzuia safari hiyo hiyo mida ya usiku, ili waweze kuzuia  msaada wa kwa mganga. Kipindi  anapelekwa kwa mganga haraka haraka usiku sana.

Walishangaa kukuta mawe makubwa na mazito sana barabarani yameziba barabara ili wasipite dooh na hakukua na njia ya pembeni ile sehemu maana juu ilikuwa ni mlima hivyo gari la yule daktali lisingeweza kupita kabisa. walipoenda kuyatoa yale mawe ili wapite maana njia nzima ilizibwa kabisa jamani. Wakati huo pia mda nao ulikuwa unaenda sana kipindi wanaangaika kuyatoa yale mawe yaliyo kuwa yamewekwa na wale wachawi.

Dakika zilikuwa zimebaki 2 tu mdogo wangu apoteze maisha yake! Mimi nilikuwa ndani ya gari na mdogo wangu niliumia sana jamani mdogo wangu aliponishika kichwani akinipungia mkono wake akiniaga kuwa anakufa, dooh kule nje Madaktari walikata tamaa palepale maana kiukweli yale mawe yalikuwa mazito sana, yaliwashinda nguvu zao na akili kabisa. Ilipo baki dakika moja mdogo wangu afe mimi tayari nilikuwa nimeisha anza kulia tayari maana damu zilianza kumtoka sikioni pamoja na jicho lake la kushoto..

Dooh ilikuwa ni simanzi na majonzi sana kwa kila mtu maana jicho lilimtoka sana mdogo wangu jamani yani jicho likawa jekundu sana, mdogo wangu masikini alianza kuachama mdogo wake akiufumbua  sana tena akiwa anajiviringisha kwa kujigalagaza maana kifo kilikuwa kinamuita sasa. Tumbo lake likikuwa kubwa sana ngozi ikawa nyepesi kiasi kwamba tulishangaa sana. watu waliumia wakasema mengi “jamani huyu dada kasoma sana. alikuwa na akili sana darasani leo hii amelogwa anakufa na elimu yake jamani dooh inauma sana hii” wakati amebakiza sekunde chache ili apoteze maisha. Radi kali sana ilipiga ghafla, tena yenye mwanga wa ajabu ambao nilikimuwa sijawai kuona maisha yangu yote.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here