SHARE

Sehemu ya 70

Kumbe ni mzimu wa mama ulikuwa umekuja kwa kasi sana kumsaidia mdogo wangu. Mzimu wa mama ukasema “siwezi kukubali mwanangu afe” Wale wachawi pia hawakukubali ndipo wakaanza kuzuia mzimu wa mama usiweze kumsaidia mdogo wangu. Dooh mama aliteseka sana maana wale wachawi walikuwa wengi na walikuwa na nguvu pia. Kipindi mama anajaribu kupambana kunusuru uhai wa mdogo wangu. Mchawi mkuu alikuja na mchanga uliyoko juu ya kabuli la marehemu mama yangu alafu akaurusha kwenye kivuri cha mzimu wa mama. Dooh mzimu mama uliishiwa nguvu kabisa. wale wachawi walicheka sana wakisema “tumekuweza sana leo umetusumbua sana we mwanamke” mama alishindwa cha kufanya kabisa, mzimu wa mama ukaondoka eneo lile. Wakati mdogo wangu anaanza kukata roho.

Wale wachawi wakaanza kufurahi wakisema “tumewashinda nguvu hawa watu wa mungu tukale nyama yake sasa huyo binti” niliumia sana kumuona kaka yake mama anashirikiana na wachawi wenzake kumua mdogo wangu. Mdogo wangu alipo anza kufumba macho sasa anaelekea kupotea nililia sana niliumia sana jamani nilisikitika maana ndiye alie kuwa tegemezi na ndiye aliekuwa msomi kwetu, kabla hajafa mala ghafla tena! Mzimu Mama danieli ulikuja  kipindi wale wachawi  hawajajipanga kabisa.

Ndipo mzimu wa mama dani ukaniambia  kwamba ” mwanangu nusuru maisha ya mdogo wako amebakiza sekunde chache afe” nikauliza nifanye “nini sasa jamani mimi, ”  mzimu wa mama danieli ukaniambia “Nyofoa nyusi moja ya mdogo wako kisha weka mdomoni mwake haraka sana” nilifanya hivyo hapohapo. Nilishangaa mdogo wangu anaamka anashangaa kafikaje pale! akashangaa pia kuona anatokwa damu bila maumivu, na mda ule mzimu wa mama ulipo shindwa nguvu na wale wachawi, Kumbe mzimu wa mama ukaenda mpaka kwenye makao makuu ya wale wachawi kisha akachoma moto vyombo vyao na mitunguri yao yote ya kishirikina na baada ya mdogo wangu kumuwekea nyusi alipona hapohapo wale wachawi walivyo ona amepona na wao wameishiwa nguvu. Walirudi haraka makao makuu yao ya uchawi kuchukua nguvu upya ila wakakuta uchawi wao tayari umeunguzwa wote na moto.

Waliumia sana walilia sana maana ata pembe lao la kichawi lilichomwa. Ndipo wakaachana na uchawi maana hawakuwa na uwezo wala nguvu  tena, waliteswa sana jamani maana wale watu wote walio watoa kafara waliwatokea sana jamani wakiwa wanalia wakiwambia wale wachawi “kwanini mlituua sisi ” na  lile jiwe tumboni mwa mdogo wangu likapotea kabisa ikarudi mimba ya ukweli ya Yule kaka yake mama wa kambo. Baada ya yule kaka kuona kapoteza uchawi na hana maisha tena akarudi kuomba msamaa kwa mdogo wangu maana uchawi wao wote uliharibika! Alirudi mdogo wangu akasema siwezi kukusamee kabisa yule kaka akasema  “naomba unisamee sio mimi nilitaka kukuua, ilikuwa ni amri nilipewa na wakuu wangu kuuwa maana  bila wewe kufa ndogo wangu angeteseka sana na ulioneka kuwa na ulinzi mkubwa maana ulipona ile dawa tulikutegea  chini ya godoro lako pia ulitoroka kwa mama dani baada ya kunusulika kifo,  naomba nisamee nimeacha uchawi sahivi tuzae mtoto tumlee pamoja”. Yule kaka alikataliwa msamaa wake akaambiwa “je ningekufa mimi mtoto ungetutoa wapi”.

Baada ya mama yangu wa kambo kuangaika sana bila kupata kazi ndipo akaamua kutafuta japo kazi za usafi.  akawa amepata kazi ya kufanya usafi ndani ya hospitali kubwa mjini na kufua mashuka na kusafisha vizuri hospitali. Maisha ya kaka yake mama wa kambo na mama wa kambo yalikuwa magumu sana waliangaika sana na maisha. Baada ya kama miezi min’ne uchungu wa kujifungua ulimshika mdogo wangu. Dooh alikuwa muoga sana maana ndiyo ilikuwa mimba yake ya kwanza, alilia sana siku hiyo akihema kwa spidi sana. Ndipo sisi haraka haraka tukampeleka hospitali. Mdogo wangu aliangaika sana kwenye kujifungua maana njia ilikuwa ndogo ikabidi aongezewe njia ili mtoto apate kupita na kuzaliwa salama. Mungu saidia mdogo wangu akajifungua salama mtoto wa kiume mzuri mwenye kilo za kutosha tu. Kumbe ile hospitali ndipo palepale masikini wa mungu!

Usikose sehemu ya 71


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here