SHARE

Bamia ni mboga ambayo inafahamika kwa wengi katika jamii kutokana na ladha yake nzuri inapotumika kama mboga katika baadhi ya milo. Mfano ugali.

Bamia kwa kawaida huwa na rangi ya kijani iliyokolea na hukua hadi kuwa na urefu wa sentimeta tano hadi 15.

Bamia imebarikiwa virutubisho vingi ikiwa ni pamoja na vitamini A ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu. Hivyo sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake.

Aidha, kwa wale wenye matatizo ya kuona, wanapokula bamia mara kwa mara huwasaidia kuimarisha mwanga katika macho yako.

Mtu mwenye wingi wa vitamini A mwilini huwa na nafasi ndogo ya kuzongwa na maradhi yatokanayo na virusi kama mafua.

Halikadhalika uteute unaopatikana katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Hivyo watu wenye ngozi laini huwa na kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia kulinda ngozi.

Mbali na hayo, pia ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu. Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here