SHARE

Baada ya miaka mitatu mama yangu wa kambo kutokana na miangaiko yake yote ya maisha mpaka kujimwagia mitindikali usoni, akajikuta anapata KANSA ya shingoni. Alizubaa kuitibu, kumbe kansa ikaenea mwilini mwake ikakomaa, hivyo basi kutibiwa kwake ikawa ngumu! maana alitakiwa kukatwa shingo kansa isienee mwilini zaidi, na kibaya zaidi, “mtu akikatwa  shingo anakufa” hivyo sasa, akaamua kukaa hivyo hivyo tu, shingo lilioza sana akavimba vibaya shingo lake.

Yani shingo likikuwa na michilizi inayo tia kinyaa ukimtazama kwa macho unajisikia vibaya yani mwili unasisimka sana, Aliendelea kukaa ndani akiwa anaoza polepole,funza na nzi vilevile na wadudu wa kila aina walimjaaa mama wa kambo tena hao wadudu wakimtembelea akiwa bado ni mzima wa afya, kibaya zaidi alikuwa ananuka pia maana alikuwa mwasilika wa ukimwi ukichanganya na magonjwa yake pia akaisha mwili kabisa, watu walishindwa kumuhudimia maana alikuwa akijisaidia sehemu aliyo lala hapohapo, hivyo alikuwa anatoa harufu Kwelikweli.

mama wa kambo alikata tamaa maana aliugua na hakuna ata mmoja alie mpelekea chakula. hakuwa na mtu wa kumpa msaada wowote, ata mimi na mdogo wangu tuliogopa kumsaidia maana tulijua ni kigeugeu sana unamsaidia leo kesho anakuua.  Ilipo fika tarehe 12/6/ siku na mda ambayo alifariki  mama danieli ndipo mama wa kambo alikata roho akafa mda huo huo pia, “kweli malipo ni hapahapa duniani”. Mimi, mdogo wangu na baba tulipo pata taarifa za msiba wote tulienda kwenye msiba wake! Ili tumzike kwa amani. tulim’wagia mchanga kabulini mwake na tukaondoka makabulini pale. Tangu ile siku mama wa kambo amekufa, tunaishi kwa amani na upendo tele, mizimu ilipumzika kwa amani na haijatutokea mpaka leo,

MWISHO WA SIMULIZI YA DAMU YA BABA.

MTUNZI  FRANK DAVID

NAMBA za simu ni

+255769510060


3 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here