SHARE

Star wa Bongo Flava Aslay ameahidi kuendelea kutoa Hit baada ya Hit hadi mwaka huu utakapomalizika kisha mwakani anaweza kuja na Album yake.

Akizungumzia ujio wa Ngoma mpya ya Aslay inayokwenda kwa jina la “Natamba” Meneja wa msanii huyo Chambuso amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kutoa burudani kwa kuachia nyimbo mpya hadi mwaka utakapomalizika ndio wanaweza kufikiria kutoa Album.

“Hii mvua ya ngoma mpya ndio kwanza imeanza, tutaendelea kutoa hadi mwaka umalizike kisha tutatazama upepo wa Januari ndio tunaweza kutoa Album kwani nyimbo zipo nyingi tu”, amesema Chambuso.

Chambuso ameongeza kuwa kwasasa hawawezi kutoa Album kwasababu soko lake limeyumba ndio maana wamewekeza zaidi kwenye kutoa Video kisha kuweka kwenye mtandao wa Youtube ili wapate malipo pamoja na kufanya Show.

Baada ya Hit kama Baby na Pusha nyota huyo ambaye awali alikuwa anatamba na kundi la Yamoto Band kabla ya kusambaratika, ataachia wimbo mpya siku ya Jumatano unaoitwa Natamba.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here