SHARE

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amefunguka kwamba ikiwa wamefanikisha kuupata ushahidi wa rushwa unavyotumika katika ofisi za umma Arusha anauhakika pia wataupata pia ushahidi wa kujua Ben Saanane alipo pamoja na aliyefanya Shambulio la Lissu.

Akizungumza jana kwenye mkutano alioufanya na wanahabari yeye pamoja Mbungea Joshua na Nassari wa Arumeru Mashariki, wakati walipokuwa wakiuonyesha baadhi ya ushahidi walionao

“Kama ambavyo hili jambo limekuwa ‘revealed kwa kiasi hichi huko mbele ya safari tunapoenda mambo ya Ben Saanane yatakuwa wazi pamoja na shambulio la Tundu Lissu. Hivyo tunapeleka ushahidi wote kwa Mkurugenzi wa Takukuru na tunamtaka achukue hatua kama jinsi alivyochukua hatua kwa Rugemalila na wengine” Lema

Aidha Mh. Lema amesema kuwa matukio yanayoendelea ndani ya Mkoa wa Arusha hayawezi kufichika kwa kuwa wao ndiyo wenye mkoa na wanajua namna gani ya kucheza michezo yote hivyo ni vyema watu hao wakachukuliwa hatua ili wasiendelee kukaa ofisini.

Kwa upande wa Mbunge Joshua Nassari amesema kwamba anajua jambo analolifanya linahatari kubwa lakini tayari ameshajitolea hata kufa kwa ajili ya kusema ukweli na kulitetea taifa

“Nimeondoka Nairobi Lissu bado ni Mgonjwa sana hawezi kufanya lolote. Najua hata sisi ndipo tunapoelekea lakini tumeshajitolea ma tupo tayari. Mimi mke wangu amelia sana leo wakati nikiwa nakuja kuutoa ushahidi huu” Nassari amesema

Mbali na ushahidi walioutoa Lema pamoja na Nassari wamesema kwamba kwa siku ya jana wametoa sehemu ndogo ya ushahidi wao na kwamba sehemu nyingi watakwenda kuzitoa Takukuru kwani ni aibu na fedheha kutoa ushahidi huo ambao wanaamini utaichafua nchi pamoja na Rais kwa ujumla.

Pamoja na hayo Mh. Lema amesema kwamba pamoja na kwamba ametoa ushahidi huo hadharani hana uhakika kama kuna hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa ingawa ana uhakika na amani kwama ameshatimiza wajibu wake.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here