SHARE

Msanii wa muziki wa singeli bongo ambaye anaendelea kupeperusha bendera vyema kwenye muziki huo, Sholo Mwamba, amesema kilichomfanya aondoke kwa bosi wake ‘Muna Love’ ni kitendo chake cha kutumia pesa hovyo wanazotafuta kwa nguvu na ‘viben ten’.

Akizungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, Sholo Mwamba amesema alikuwa anakwazika sana kitendo cha wao kwenda kufanya show mikoani na kuleta pesa kwa bosi, na matokeo yake yeye pesa anatumia na wanaume wengine ambao ni wadogo ki-umri huku akiwataja wengine ambao ni wasanii Dogo Janja na Young Dee.

“Kitu ambacho kimenudhi na sijakipenda zaidi kwa Muna ni kitendo cha sisi watoto wa kiume tunaenda kutafuta hela halafu tunawakuta madogo wengine wamekaa wamejiachia, sisi wahuni ndo tunaunga tunaenda kuimba visingeli vijijini tunaleta mpunga kwa bosi alafu anatumia na wajinga, tunaona miyeyusho”, amesema Sholo Mwamba.

Pamoja na hayo Sholo Mwamba amemtaka Muna Love kuacha mambo hayo na atunze familia yake, ili siku moja washuhudie harusi yake, na sio kujichanganya na watoto wadogo


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here