SHARE

MAPENZI sanaa tamu ya wakubwa. Lakini hugeuka kuwa chungu kama shubiri pale unayempenda mnaposhindwana, anakutenda au mnaachana. Katika ulimwengu wa leo, kutokana na utandawazi na watu wengi kutokuwa waaminifu katika uhusiano wao wa kimapenzi, kila kukicha kumekuwa na vilio vya wapenzi kusalitiana kisha kuvunja uhusiano au ndoa. Katika makala haya nakuletea baadhi ya mastaa wa kike ambao licha ya kuwa warembo na kila mwanaume rijali akiwaona, lazima awamezee mate, lakini wamejikuta wakiteswa na mapenzi na kubaki wakiumia na kulia kila kukicha kwani wanapopenda wanajikuta wakishindwana.

ZARINAH HASSAN ‘ZARI’
Mwanamama huyu raia wa Uganda ni mrembo hasa, kwani licha ya kuwa ni mama wa watoto watano, lakini bado yupo vizuri na ni miongoni mwa warembo wanaovutia kwa macho. Zari amepitia misukosuko mingi ya mapenzi hadi kuachana na aliyekuwa mumewe, marehemu Ivan Ssemwanga aliyezaa naye watoto watatu kabla ya kuangukia kwa staa wa Bongo Fleva ambaye wamejaaliwa watoto wawili. Licha ya hao, pia aliwahi kusemwa kutoka na mmoja wa marafiki wa karibu wa Ivan, King Laurence na pia hivi karibuni kudaiwa kutoka na mmoja wa vijana wanaosaidia mazoezi yake Gmy, ambaye nusura amtenganishe na baba wa watoto wake wawili. Hivi karibuni Zari amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya Mbongo Fleva huyo kuchepuka na kuzaa na mwanamitindo, Hamisa Mobeto hali iliyosababisha watu kumtukana huku wengine wakimtia moyo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

JACQUELINE WOLPER
Mwanadada huyu mrembo amepitia misukosuko mbalimbali katika mapenzi kwani aliwahi kuvishwa pete ya uchumba na mwanaume mmoja raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuachana. Haikuishia hapo, aliwahi kuchumbiwa na mfanyabiashara, Abdallah Mtoro ‘Dallas’, lakini
uhusiano wao uliyeyuka, akarejea kwa Mkongo mwingine kabla ya kuingia kwa msanii wa Bongo Fleva ambaye alimtambulisha hadi ukweni kwao huko Mtwara, lakini walimwagana na sasa yupo na mwanaume mwingine anayejulikana kwa jina moja la Brown.

WEMA ISAAC SEPETU
Miss Tanzania huyu wa mwaka 2016, mapenzi yamekuwa ni kitendawili kwake kwani amewahi kuwa kwenye uhusiano na wanaume mbalimbali. Huyu, pengine ndiye staa mwenye kujua hasa maumivu ya mapenzi kwa sababu orodha ya wanaume aliowahi kutoka nao, inatisha! Mr Blue, TID, Charlz Baba, Steven Kanumba, Kigogo wa Ikulu, Mkongo na wengineo ni baadhi ya watu ambao wamewahi kushiriki mapenzi na kumwagana na mrembo huyu matata. Pia aliwahi kuwa na staa mkubwa wa Bongo Fleva na baada ya hapo akaingia kwenye uhusiano na Mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan kisha wakatemana. Hivi karibuni ameripotiwa kuwa kwenye uhusiano usio wa ‘matangazo’ na mfanyabishara wa Arusha.

KAJALA MASANJA
Staa huyu ni mrembo, lakini na yeye ameonja maumivu makali ya mapenzi. Baada ya kuingia kwenye uhusiano wa mapenzi na prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthyase ‘P Funk’ na kujaliwa kupata mtoto wa kike, Paula, hatimaye walitemena licha ya kukaa kwa muda mrefu. Haikuishia hapo, aliingia kwenye ndoa na kijana Faraji Chambo lakini ndoa yao iliingia doa baada ya Chambo kutiwa nguvuni na vyombo vya dola kwa matatizo kadha wa kadha. Baada ya kuachana, akaingia kwenye uhusiano na msanii Quick Rocka, kabla ya kusemwa kuwepo katika uhusiano na mwanaume mwingine kwa sasa. Ni mwanamke ambaye ana
historia ya kusisimua katika chungu na tamu ya mapenzi.

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’
Mwanamama huyu, licha ya kuwa na watoto wawili, bado ni mrembo, amewahi kuwa kwenye uhusiano na wanaume tofauti, lakini hadi sasa hajapata wa kumuoa. Shilole amewahi kuwa kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda ambaye alimvisha hadi pete ya uchumba, lakini matokeo yake alikwenda kumuoa mwanamke mwingine. Pia amewahi kuripotiwa kuwa na Wabongo Fleva, Elias Barnaba, Boy Caro, Neddy Music na sasa yupo na Uchebe ambaye aliwahi kukiri kwamba amesha-mtolea posa na ndoa yao itakuja ‘soon’.

HAMISA MOBETO
Ni mrembo, mama wa watoto wa wawili ambapo mwanaye wa kwanza alizalishwa na bosi mkubwa wa kituo cha redio, akamwagwa. Hivi karibuni mwanamama huyo ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuripotiwa kuzaa na msanii mkubwa wa muziki wa kizazi kipya, lakini uhusiano wao, licha ya kupata naye mtoto, unaonyesha ni mchungu kwake kwani haionekani kama atapata alichotegemea


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here