SHARE

Hali si shwari kati ya wasanii wawili TID wa bongo na Prezzo wa Kenya, baada ya wawili hao kurushiana maneno ambayo yalionekana kumkera mmoja wapo kisa kikiwa ni Amber Lulu.

Balaa limeanza pale ambapo TID alimshauri Prezzo kutumia kinga tena ya gharama zaidi, iwapo anajihusisha kimapenzi na Amber Lulu, kitendo ambacho kimemchukiza Prezzo.
“Prezzo kula bata mwanangu fanya mambo na Amber Lulu, Prezzo pole sana jiongeze mtu wangu, tumia mpira (condom) ya gharama zaidi ambayo hujawahi kutumia kabla, kwa sababu sehemu unayokwenda ni moto”, amesema TID.
Kauli hiyo ya TID imeonekana kumkera Prezzo na kusema kwamba hakukuwa na haja ya kuyapeleka kwenye TV.
“Namshangaa mshkaji wangu, kuna watu huwa wananiingia kwa kona mbaya, ukiingia kwa kona mbaya mimi ni msela nitakuzingua, kitu ambacho sijafurahia ni kwenda kutangaza kwenye TV, yeye ni mshkaji wangu angenipigia simu akaniambia, na sio kuniharibia ‘mood’ yangu”, amesema Prezzo.
Prezzo amekuwa hapa nchini takriban wiki, na amekuwa akionekana na msani Amber Lulu akiwa naye kwenye chumba cha hoteli, kitendo ambacho kimeibua gumzo kwa mashabiki wengi.


1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here