SHARE
Barcelona's midfielder Andres Iniesta holds up the cup after the team won the Spanish Copa del Rey (King's Cup) final football match FC Barcelona vs Deportivo Alaves at the Vicente Calderon stadium in Madrid on May 27, 2017. Barcelona won 3-1. / AFP PHOTO / Josep LAGO (Photo credit should read JOSEP LAGO/AFP/Getty Images)

Andres Iniesta amezima tetesi zote zilizokuwa zikiuzingira mustakabali wake kwa kusaini mkataba mpya Barcelona.

Iniesta, 33, angekuwa mchezaji huru majira ya joto 2018, kwani mkataba wake ulikuwa unakwisha Cam Nou.

Sintofahamu ya muda mrefu iliyodumu Katalunya ilizipa klabu nyingine fursa ya kuanza kuzungumza na mchezaji huyo.

 Hata hivyo Iniesta alitoa habari njema mwishoni mwa mwezi Septemba kuwa mazungumzo yalikuwa yakiendelea baina yake na klabu.

Barcelona sasa wametangaza kuwa makubaliano yamefikiwa taarifa kutoka tovuti rasmi ya klabu ikisomeka: “Andres Iniesta amesaini mkataba wa maisha na FC Barcelona Ijumaa, dili litakalomweka klabuni hapo kipindi chote cha soka lake.

“Kiungo huyo wa Hispania, ambaye amecheza mechi 639 Barca, ni mchezaji wa pili kucheza mechi nyingi wa muda wote klabuni hapo.

“Amefunga magoli 55 kwenye timu ya kwanza, tangu alipoanza kucheza Oktoba 29, 2002.

“Tangu 2015 Iniesta amekuwa nahodha wa kikosi cha kwanza na ni miongoni mwa wachezaji ambao ni kama nembo ya klabu.

“Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na klabu Septemba 1996, akiwa na miaka 12.

“Iniesta na Leo Messi wana rekodi moja ya kutwaa mataji mengi zaidi katika historia ya Barce, 30.”


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here