SHARE

Account ya YouTube ya Aslay ambayo ilihakiwa na watu na kuiwekea vikwazo kwa watu wanaotaka kutazama kazi zake, imerudishwa baada ya kuhangaika nayo kwa muda mrefu.

Taarifa ya kurudishwa kwa account hiyo imetolewa na mmoja wa mameneja wake Mx Carter ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mitandao na mpiga picha maarufu hapa bongo, kupitia ukurasa wake wa twitter.

Kwenye taarifa hiyo Mx Carter ameandika ‘Usiyempenda karudi”, na kuweka picha ya Aslay.

Leo asubuhi Mx Carter alitoa taarifa kuwa account hiyo imehakiwa, na kuwataka watu kuwa wapole wakati wanahangaikia kuirudisha.

Hivi karibuni Aslay amekuwa msanii ambaye anafanya vizuri zaidi mtaani kwa kutoa kazi kali mara kwa mara, na hivi juzi kaachia video yake mpya ya ‘Natamba’.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here