SHARE

Andres Iniesta amewataka viongozi wa Barcelona kuhakikisha Lionel Messi anasaini mkataba mpya kwani klabu “haiwezi kuishi bila yeye”.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina bado hajajifunga rasmi na miamba wa Catalan, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kufika tamati mwishoni mwa msimu.

Lionel Messi Andres Iniesta BarcelonaRais wa Barca Josep Maria Bartomeu amesisitiza mara kadhaa kuwa ni swala la muda tu tangazo litatolewa, lakini Iniesta – ambaye binafsi amesaini Ijumaa mchana anataka tetesi zikome kabisa.

“Kwa swala la Leo nadhani hakuna shida katika swala la mazungumzo,” aliwaambia waandishi. “Klabu inamhitaji Leo, anahitaji kuwa hapa. Natumai habari zake [katika Barca] hazitakoma.

“Ni wa kipekee, hatuwezi kuishi bila yeye na nadhani klabu inafikiri namna hiyo hiyo. Ni swala la muda tu, lakini natumai atasaini mkataba mpya mapema iwezekanavyo.”

Iniesta amefuta shaka zote juu ya mustakabali wake Barcelona baada ya kukubali kusaini mkataba wa “maisha” Camp Nou.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here