SHARE

KUWA profesa ni moja ya mafanikio ya kitaaluma ambayo mtu huweza kuyafikia. Pamoja na kuwepo kwa mamilioni ya tafiti za ngazi ya PhD zilizoidhinishwa katika dunia hii bado hakuna mipaka kwa kile ambacho ubongo wa binadamu unaweza kufikia.

Tunaelewa kuwa kutunikiwa cheo cha profesa si jambo rahisi lazima mtu aonyeshe uwezo wake wa kiakili ambao unasababisha matokeo chanya katika ulimwengu huu.

Maprofesa hupewa heshima maalumu katika kazi wanazofanya na hulipwa mishahara minono kulingana na kazi hizo.

Kuna maprofesa ambao hulipwa fedha nyingi kuliko wengine kutokana na ukarimu, ujuzi na vipaji vyao ambao wengi wao wamebadilisha ulimwengu kwa kutumia taaluma zao.

Kutoka kwenye vitabu vinavyotumiwa darasani hadi katika ulimwengu wa uvumbuzi wao si kurudia ugunduzi uliyofanyika ila wao kufanya uvumbuzi kueleweka kwa urahisi katika matumizi.

Wiki hii tunangalia wanataaluma au maprofesa wanaolipwa mishahara mikubwa kila mwezi duniani kwa mwaka 2017.

David Silvers (Dola milioni 4.33)

Profesa David Silvers raia wa Marekani mwenye asili ya India anaongozwa kwa kulipwa mshahara mkubwa kwa mwaka huu.

Profesa huyu mwenye taaluma ya udaktari wa asili ya magonjwa (Pathology Dermatology) katika Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani hulipwa mshahara wa dola za milioni 4 kwa mwezi.

Alisoma masuala ya Dermatology katika Chuo Kikuu cha Duke mwaka 1968 nchin Marekani. Profesa huyu amegundua mambo mengi na kazi zake zinaheshimiwa na kujulikana duniani kote.

Zev Rosenwaks (Dola milioni 3.3)

Dk. Zev Rosenwaks ni profesa wa magonjwa ya uzazi kwa wanawake (Gynecologist) na raia wa Marekani, utafiti wake wa udaktari uliidhinishwa na Chuo Kikuu cha Cornell.

Vyeti vyake vya taaluma ya uzazi vinamwezesha kufanya kazi mahali popote duniani.

Profesa Rosenwaks ni mvumbuzi wa teknolijia ya kupandikiza mbegu za mwanamume kupitia maabara inayojulikana In Vitro Fertilization (IVF) nchini Marekani, hasa katika taasisi ya madawa na uzazi ya Jones Institute of Reproductive Medicine, pia alianzisha mfumo wa kampeni ya kuchangia au kutoa yai la uzazi nchini Marekani. Zev Rosenwaks hupokea mshahara wa dola milioni 3.3 kila mwezi.

Dean Takahashi (Dola milioni 2.6)

Profesa Dk. Dean Takahashi wa Chuo Kikuu cha Yale nchini Merekani ni mkuu wa fedha katika chuo hicho. Ana shahada ya PhD ya uchumi pia ni mkurugenzi wa uwekezaji chuoni hapo.

Takahashi husimamia matumizi ya fedha za mpango wa pensheni wa chuo kikuu wenye thamani za dola bilioni 17, alikuwa mfanyakazi wa zamani katika idara ya uwekezaji katika jiji la Boston, Marekani. Profesa huyu ni mzaliwa wa India lakini sasa ana uraia wa Marekani

William Fruhan (Dola milioni 1.19)

Chuo cha Biashara cha Harvard kinamlipa profesa Dk. William Fruhan, dola milioni 1.9. Ni profesa wa msingi katika chuo hicho, pia awali alikuwa mwalimu msaidizi baadaye akawa mwenyekiti wa idara ya usimamizi wa juu.

Alipata PhD akiwa Harvard na amechangia katika mafanikio ya mashirika 15 tofauti na pia ni mwandishi wa masuala ya fedha. Fruhan ni Mmarekani mwenye asili ya India.

Dan Laughhunn (Dola milioni 1.03)

Milionaire professor Dan J. Lauhhunn anayejulikana kama genius kati ya maprofesa wastaafu. Mmarekani huyu mwenye asili ya India, alipata PhD katika chuo cha Illinois nchini Marekani katika masuala ya biashara na utawala na anafundisha katika chuo cha Duke nchini Marekani.

Profesa huyu ni mtaalam wa uchumi katika kupanga bajeti na usimamizi. Utafiti wake katika nadharia za biashara umesababisha mafanikio na hutumika na makampuni makubwa duniani.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here