SHARE

Beki wa Manchester United Matteo Darmian amebainisha kuwa anamchukulia David de Gea kama kipa bora duniani, mbele ya Muitaliano mwenzake Gianluigi Buffon.

De Gea amefurahia mwanzo mzuri msimu huu, akicheza mechi saba bila kuruhusu goli baada ya kucheza mechi tisa Ligi Kuu Uingereza na Ligi ya Mabingwa, wakati Buffon akiendeleza umahiri Juventus.

Darmian anaamini Buffon, 39, ni kipa bora wa muda wote, lakini beki huyo anahisi De Gea ndiye mwenye kiwango safi kwa sasa

┬áDarmian, 27, aliiambia tovuti rasmi ya klabu yake: “Namfahamu David vema na nadhani, kwa sasa, ndiye kipa bora duniani. Ni mtu muhimu sana kwetu na nadhani hatari aliyookoa Stoke (Kutoka kwa Jese Rodriguez) ilikuwa nzuri sana.

“Nadhani Gianluigi ni kipa bora wa muda wote. Pia ni mtu mwema. Kwa hiyo naweza kusema nina bahati kucheza na makipa mahiri kama hawa.

“Naam, wanakaribiana. Lakini sijui. Nadhani David ni kipa bora duniani na Gianluigi ni kipa bora wa muda wote. Nadhani wote wanafanana kwa sababu wapo thabiti na wanaokoa hatari golini. Lakini pia wana wasifu mzuri.”

De Gea, ambaye amekuwa United tangu 2011, mara kadhaa amehusishwa na tetesi za kutaka kwenda Real Madrid.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here