SHARE

Mwanamitindo maarufu Bongo, Calisah, ambaye hivi karibuni ameshangaza ulimwengu kwa kupiga picha akiwa amevaa viatu vya kike, amefunguka kuwa yeye ni mfanyabiashara kwa hiyo yuko tayari hata kupiga picha na gauni endapo atalipwa dau la shilingi milioni kumi.

Calisah ambaye kwa sasa ameganda kama ruba midomoni mwa watu kutokana na picha hizo, alisema “Siwezi kukataa Mkwanja kwa kuhofia watu wataongea, kitendo cha kuvaa viatu na kupiga navyo picha wala siyo vibaya, ingekuwa nazurura navyo mitaani hapo sawa. Waendelee tu kuongea mimi naingiza mtonyo na siyo viatu tu, mtu yeyote atakayeweza dau langu la milioni 10, hata gauni nitavaa.”

Pia mwanamitindo huyo alisema kuwa baada ya picha hizo kusambaa mitandaoni, familia yake ilichukia sana kiasi cha kumweka ‘kitimoto’ kwenye ‘Whatsapp Group’ la familia, kitu ambacho kilimuumiza sana, ila ilifika muda wakamuelewa.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here