SHARE

Imeripotiwa kuwa Paris Saint-Germain imedhamiria kutumia fedha kusuka kikosi chao kwa kutoa paundi milioni 90 kumsajili kiungo wa Chelsea N’Golo Kane majira ya joto msimu ujao.

Kante, 26, aliingia moja kwa moja kwenye timu ya Antonio Conte alipotua Stamford Bridge kutoka Leicester City kwa kiasi cha takribani paundi milioni 30 mwaka 2016.

PSG walimfanya Neymar kuwa mchezaji ghali zaidi duniani katika ulimwengu wa soka walipomnunua kutoka Barcelona kwa kiasi kinachokaribia paundi milioni 200, na pia waliinasa saini ya Kylian Mabppe ambaye wataweza kumpa usajili wa kudumu mwisho wa msimu huu kwa kitita kisichopungua paundi milioni 100.

 Kwa mujibu wa Le Parisien, Miamba hao wa Ufaransa wanataka kuimarisha safu yao ya kiungo kwa kusajili mchezaji mwenye kaliba ya Kante, na wapo tayari kutumia fedha nyingi kumpata nyota huyo wa Chelsea.

Mkataba wa Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa London Magharibi utafika ukomo wake 2021.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here