SHARE

Waandishi wa habari hapa nchini wametakiwa kundika habari zitakazoleta mabadiliko kwa wananchi na serikali.

Wito huo umetolewa katika mafunzo ya uandishi wa habari za mazingira yaliyoandaliwa na umoja wa klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania-UTPC- yanayofanyhika mkoani Dodoma ambayo yameshirikisha waandishi wa habari kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo meneja mafunzo na ufatiliaji –UTPC- Victor Maleko amesema waandishi wanaweza kuleta mabadiliko hasa katika uandishi wa habari za mazingira ikiwemo kuripoti kwa kina na kufuatilia kwa kiwango kikubwa habari zote zinazohusu mazingira.

Alisema waandishi wa habari ni kioo cha jamii ambacho kina uwezo wa kumulika na kuangalia matatizo mbali mbali yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira kama vile ukataji miti hovyo kuchoma misitu na kuharibu vyanzo mbali mbali vya maji.
Aidha maleko amesema –UTPC-itaendelea kutoa mafunzo mbali mbali kwa wanachama wa klabu zote nchini wenye sifa ambapo amesema mafunzo hayo yataendelea hadi mwaka 2020.

Akizungumza mkufunzi wa mafunzo hayo Deodatus Mfugale amewataka waandishi kuchagua sehemu moja kwa ajili ya kujijenga kuliko kutokuwa na upande maalum ambao anaegemea.

,,Mwandishi anatakiwa awe na sehemu maalum ambayo atajikita kwa ajili ya kuelimisha jamii kama unaandika habari za afya hakikisha unaifatilia kwa undani kuliko kujichanganya mara leo afya kesho mazingira kesho kutwa habari za uchunguzi namna hiyo huwezi kufika,,Alisema mfugale.

Mafunzo hayo ni ya siku tano yanafanyika mkoani Dodoma ambapo yameandaliwa na umoja wa klabu za waandishi wa habari hapa nchini –UTPC.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here