SHARE

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wana kikosi bora na kipana ila bado kuna shida ya uendeshaji.

Hans Poppe amesema kikosi cha Simba kinahitaji utulivu katika kukipanga na lazima benchi la ufundi lifanye kazi.

“Inawezekana katika upangaji wa kikosi kukawa kunatupiga chenga lakini kikosi kimekamilika.

“Kama unakumbuka wakati ule alipoumia Mwanjale tulihaha sana. Lakini sasa kila upande umekamilika na mchezaji zaidi ya mmoja mwenye ubora wa juu.

“Hii pia inasaidia kuongeza ushindani ndani ya kikosi lakini lazima benchi la ufundi lifanye kazi nzuri kuhakikisha upana na ubora wa kikosi unakuwa na faida.

“Sisi hatutaki kuingilia kazi yao lakini vizuri tukapata matokeo ndiyo jambo tunalohitaji,” alisema Hans Poppe.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here