SHARE

Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amesema uhakiki wa vyeti ni changamoto aliyokumbana nayo alipokuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na hataweza kuisahau ingawa anashukuru jinsi alivyopata ushirikiano.

Mh. Kairuki amesema hayo jana wakati wa kukabidhi ofisi kwa Waziri mpya wa Utumishi George Mkuchika aliyeteuliwa na kuapishwa mwanzoni mwa wiki hii ambapo amesena kwamba japo kazi hiyo ya changamoto ilichukua muda mrefu hadi kufikia kuwakatisha tamaa watumishi wa umma lakini aliimaliza vizuri.

“Nchi kama vile Afrika Kusini, India na Pakistan walifanya jambo kama hili kwa awamu mpaka nne na bado hawajamaliza, lakini sisi tumelifanya kwa jumla ingawa imechukuwa muda mrefu mpaka watumishi wakaanza kukasirika na haikuwa kazi nyepesi,” amesema.

Pamoja na chanmgamoto hiyo Kairuki amesema baadhi ya watendaji alioshirikiana nao hawakuwa waaminifu ambao walipenyeza watu wasiokuwa na sifa jambo ambalo amemtaka Waziri Mkuchika kupambana nao ipasavyo.

Aidha ameongeza kwamba suala la maslahi ya watumishi wa umma lilikuwa changamoto nyingine kwa sababu serikali inatamani kuyaboresha lakini fedha inayokusanywa haikidhi mahitaji.

Mbali na hayo amewatoa shaka watumishi ambao hawajapandishwa madaraja akifafanua kwamba fedha kwa ajili watumishi zaidi ya 163,000 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza suala hilo la maboresho.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here