SHARE

Kylian Mbappe ameonyesha kuwa ni mtaalamu zaidi ya Lionel Messi alivyokuwa katika umri wa miaka 18, kwa mujibu wa Ludovic Giuly aliyewahi kucheza kikosi kimoja na nyota huyo wa Barcelona.

Mbappe, 18, anatabiriwa kuwa mchezaji bora zaidi duniani baada ya kuwa na mwanzo mzuri katika msimu wa 2016-17 akiwa na Monaco, jambo lililozivutia klabu nyingi za Ulaya.

Paris Saint-Germain walishinda vita hiyo kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa na kumchukua kutoka Monaco kwa mkopo wakiwa na fursa ya kumpa mkataba wa kudumu msimu ujao, dili litakalowagharimu takribani euro milioni 180.

Mshambuliaji huyo tayari ameshafunga magoli matatu katika mechi sita kwenye michuano yote akiwa PSG na Giuly amedai kuwa amekuwa na maendeleo ya haraka zaidi hata ya Messi alivyokuwa Barcelona.

“Kylian ni mtu muhimu sana,” Giuly, nyota wa zamani wa PSG alikiambia RMC. “Ana vigezo vyote vya kuwa mchezaji mkubwa, ni mtaalamu na mwenye weledi. Aliichague PSG ili aweze kukua.

“Mbappe ni mtaalamu zaidi ya Messi katika umri wake. Anajua vema namna ya kuutawala mwili wake. Leo alikuwa na hofu nyingi na afya yake wakati alipokuwa anakua. Hali ilikuwa tata kwake.

“Kylian ana faida ya kujitambua na anakuwa vizuri.”

Messi aliwasili Barca akiwa na umri wa miaka 13 na alipewa tiba ya homoni za ukuaji kutibu mapungufu aliyokutwa nayo akiwa Argentina.

Baada ya kuingia kikosi cha kwanza akiwa na umri wa miaka 16, mshambuliaji huyo amefanikiwa kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa kadhalia tuzo tano za Ballon d’Or akiwa na klabu hiyo ya Catalan.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here