SHARE

Kiungo wakimataifa wa Simba Haruna Niyonzima, amewataka wachezaji wenzake kuamka na kucheza kwa kujituma ili waweze kushinda mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Kagera Sugar.

Niyonzima amesema , huo ni mchezo mgumu ambao wanatakiwa kucheza kwa kupambana ili kuweza kupata matokeo vinginevyo wanaweza kujikuta wakiwa katika hali mbaya wasiyotegemea.

“Ligi ni ngumu na hakuna timu nyepesi msimu huu, hivyo nilazima tupambane kuonyesha ubora wetu na kuipaisha Simba iweze kukaa kwenye nafasi yake kwenye msiamo wa ligi,”amesema Niyonzima.

Kiungo huyo wa zamani wa Yanga amesema kitu cha msingi wanachotakia kufanya ni kucheza kwa juhudi katika kila mechi bila kudharau udogo wa timu hilo linaweza kuwasaidia kuweza kutimiza malengo yao.

Amesema sababu kubwa ya Yanga kutawala soka la Tanzania kwa misimu minne iliyopita ni kutodharau timu ndiyo maana waliweza kufanya vizuri ndani na nje ya nchi sasa hilo kama likihamishiwa Simba litakuwa jambo zuri kwasababu timu hiyo inawachezaji wenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja.

Niyonzima pamoja na nyota wengine wa Simba wanadeni kubwa kwa mashabiki wa timu yao, kubwa ni kuipa ubingwa wa Tanzania bara, na kutetea taji lao la Kombe la FA, lakini pia kufika hatua za mbali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika watakayoshiriki mwakani.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here