SHARE

SEHEMU YA PILI

“Kijana hebu tueleze hali ambayo imetokea pengine tunaweza kusaidiana mawazo na jambo likawa jepesi” aliongea mzee mmoja wa makamo ambaye sikumfahamu ila moja kwa moja nikajua Mangi alimuita ili kuja kusaidia baada ya kuniona katika hali ile isiyoeleweka. Nilijikaza nikawasimulia mkasa uliotokea, wakati naendelea kuongea watu walikuwa wanazidi kuongezeka.. mpka namaliza kuongea kulikuwa na kundi kubwa sana, wake kwa waume. “Jamaniiiii hali hii mpaka lini?”
ilikuwa sauti ya mama mmoja mtu mzima ambaye alikuwepo akisikiliza maelezo yangu, kauli ile iliniacha njia panda.. inamaana matukio ya namna hii ni yakawaida kutokea eneo lile? Nilikuwa nikijiuliza. Watu ambao walikuwepo pale pia hawakuonekana kujiuliza ni wapi alipotelea
mke wangu badala yake walionekana kunionea huruma. Pemebeni nilimuona mzee yule ambaye alinitaka kuwaelezea ambacho kilinisibu akishauriana na wanaume wengine watatu kisha wakaja pale nilipo..
“Tumpelekeni kwa mzee Miale” aliongea yule mzee, wakanisaidia kunyanyuka na safari ya kuelekea kwa Mzee Miale ambaye sikujua ni nani wala tunaenda kufanya nini kwake ikaanza. Kwakweli nilikuwa
nimechanganyikiwa nikajikuta nafuata kila ambacho naambiwa bila hata kuhoji.
Tulifika kwa mzee Miale tukabisha hodi na kupokelewa na mama mtu mzima kidogo.
“Karibuni jamani, kwema?” alitukaribisha mama yule akiwa na mshtuko nadhani ilitokana na wingi wa watu ambao tulikuwa tumeongozana nao.
“Sio kwema sana shemeji, huyu bwana tumemkuta?” aliongea mzee mmoja kwa niaba ya kundi lile.
“Hapana, huyu bwana ameenda kwenye
shughuli zake huko Michese ila atarudi asubuhi” alijibu yule mama ambaye nilikuwa nimegundua kuwa alikuwa mke wa mzee Miale. Yule mzee ambaye tulikuja naye akamchukua yule mama wakaa kando kidogo na kuongea, nadhani alikuwa akimuhadithia kilichonikuta. Baada ya muda
mfupi wakasogea ambapo tulikuwa tumesimama na yule mama akaongea..
“Pole kwa yaliyokukuta mwanagu, jikaze ndio ukubwa huo” akanitizama, nikaitikia kisha akaendelea “sasa wewe nenda kapumzike kesho mida ya saa mbili uje mzee atakuwepo” aliongea yule mama nami nikaitikia tukaondoka njiani tukigawanyika kila mmoja akishika njia ya kuelekea
kwake mpaka nikabaki na vijana wawili ambao tuliendelea kuongozana..
“Pole sana kaka, mimi ni jirani yako bwana, nakaa ile nyumba yenye rangi ya kijani kulia mwa pale kwako” aliongea mmoja wa wale vijana wenzangu huku mwingine akituaga na kufuata njia ambayo ilimuhusu.
“Asante aisee” nilimjibu tukaendelea na safari huku nikijaribu kudodosa juu ya ambacho anadhani kitakuwa kimepata mke wangu.
“Mimi ni mbumbumbu juu ya hili kama ulivyo wewe, ukifika kwa yule mzee kesho nadhani unaweza kupata majibu mazuri” alinijibu wakati huu tukiwa
tumefika kwangu tukaachana.
Nilitembea hatua chache kuelekea ulipo mlango wa kuingilia nikakumbuka kuwa mlango ulikuwa umefungwa na funguo alikuwa nazo mke wangu,
nikafikiri kwa muda na kisha kuamua kuwa kama simu iliachwa pale basi pengine na funguo ipo maeneo yale ila sikuiona kwakuwa kulikuwa na
giza, hivyo nikaamua kurudi eneo lile nikaitafute kwa kutumia tochi ya simu ya mke wangu ambayo ilikuwa na mwanga mzuri tu. Saa kwenye simu
ilikuwa inaonesha kuwa ni majira ya saa sita kasorobo usiku, nikatembea polepole kuelekea eneo ambalo alipotelea mke wangu, nikafika na kuwasha tochi ya simu kisha nikaanza kuangaza kuitafuta
funguo ya mlango wa nyumbni kwangu lakini nilishtushwa sana na ambacho nilikiona kama hatua tatu mbele ya ambapo nilikuwa nimesimama,
zilikuwa ni nguo za mke wangu……

Usikose Sehemu ya Tatu


2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here