SHARE

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka jioni ya leo kwa mafungu kuelekea Bukoba ambapo Jumamosi wataikabili Kagera Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, utakaopigwa uwanja wa Kaitaba.

Meneja wa Yanga Hafidh Salehe, amesema kundi la kwanza litaondoka saa 10, jioni ya leo na litakwenda kulala Mwanza kabla ya kesho kuunganisha na ndege kwenda bukoba na kundi la pili litaondoka Dar es Salaam kesho alfajiri likielekea moja kwa moja Bukoba.

“Sababu ya kushindwa kuondoka kwa pamoja ni kutokana na kukosa ndege ya pamoja, lakini hiyo siyo mbaya kwasababu kitu cha msingi ni kufika kituoni Bukoba, na limewezekana kilichobaki ni kuhakikisha tunacheza na kupata ushindi kwenye mchezo huo,”alisema Salehe.

Kiongozi huyo amesema wanakwenda Bukoba, bila ya mshambuliaji wao Donald Ngoma aliyeumia nyama za baja kwenye mchezo uliopita dhidi yaMtibwa Sugar, lakini pia bado kuna wasiwasi ya kumkosa kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko, ambaye leo asubuhi alionekana akifanya mazoezi ya peke yake.

Meneja huyo amesema kitu kizuri kwao ni kurejea kundini kwa mshambuliaji wao tegemeo Amissi Tambwe, ambaye atakuwepo kwenye msafara huo wa kikosi cha Yanga ambacho kinashika nafasi ya sita kwneye msimamo baada ya kucheza mechi tano na kushinda mbili huku ikienda sare mechi tatu.

Mbali ya kumkosa Ngoma wachezaji wengine ambao watakosekana kwenye kikosi cha Yanga ni kipa namba tatu Ramadhani Kabwili na kiungo mshambuliaji chipukizi Said Mussa ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes’.

Meneja wa Yanga Hafidhi Salehe, ameiambia Goal, kundi la kwanza litaondoka saa 10, jioni ya leo na litakwenda kulala Mwanza kabla ya kesho kuunganisha na ndege kwenda bukoba na kundi la pili litaondoka Dar es Salaam kesho alfajiri likielekea moja kwa moja Bukoba.

“Sababu ya kushindwa kuondoka kwa pamoja ni kutokana na kukosa ndege ya pamoja, lakini hiyo siyo mbaya kwasababu kitu cha msingi ni kufika kituoni Bukoba, na limewezekana kilichobaki ni kuhakikisha tunacheza na kupata ushindi kwenye mchezo huo,”alisema Salehe.

Kiongozi huyo amesema wanakwenda Bukoba, bila ya mshambuliaji wao Donald Ngoma aliyeumia nyama za baja kwenye mchezo uliopita dhidi yaMtibwa Sugar, lakini pia bado kuna wasiwasi ya kumkosa kiungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko, ambaye leo asubuhi alionekana akifanya mazoezi ya peke yake.

Meneja huyo amesema kitu kizuri kwao ni kurejea kundini kwa mshambuliaji wao tegemeo Amissi Tambwe, ambaye atakuwepo kwenye msafara huo wa kikosi cha Yanga ambacho kinashika nafasi ya sita kwneye msimamo baada ya kucheza mechi tano na kushinda mbili huku ikienda sare mechi tatu.

Mbali ya kumkosa Ngoma wachezaji wengine ambao watakosekana kwenye kikosi cha Yanga ni kipa namba tatu Ramadhani Kabwili na kiungo mshambuliaji chipukizi Said Mussa ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here