SHARE

Diwani wa kata ya Sombetini mkoani Arusha, Ally Bananga (CHADEMA) amewataka madiwani waliopo ndani ya chama chao wanaotaka kuhama waondoke mapema kwani wakigundulika ni wasaliti kipindi cha uchaguzi watawatawanya viungo.

Bananga amesema hayo huku kukiwa na mfululizo wa matukio ya madiwani wa CHADEMA kuhama kwa tuhuma za kupokea rushwa, ambapo ameweka wazi kwamba anaamini CHADEMA hawana tatizo madiwani kuhama chama, kwani ni uhuru kama ilivyo kwa mashabiki wa Timu ya Simba kwenda Yanga kwa ajili ya maslahi yao.

“Sina tatizo kwa madiwani kuhama hata kidogo, lakini kama ni kuhama kwa kununuliwa kama hivi tunavyoona hili ni tatizo na kama huna imani na sisi ondoka mapema kwa amani kwani sisi tunaelekea kwenye uchaguzi na tunaamini tutashinda kata zote”,. amesema Bananga

sasa isije ikatokea mbeleleni tukakugundua kwamba wewe ni msaliti maana tutatawanyana viungo kitu ambacho siyo kizuri. Ondokeni kwa amani yote sasa hivi mapema” – Bananga.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here