SHARE

Kwa mara ya kwanza tangu Tanganyika na Zanzibar kuungana ,kilele cha maadhimisho ya mwenge wa uhuru kwa mwaka huu zitaadhimishwa visiwani Zanzibar katika mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 14 mwezi huu.

Akizungumza na wanahabari hii leo ,Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharib Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kuwa mgeni rasmi katika siku hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli.

Aidha Mhe Ayoub amesema kuwa pamoja na tukio hilo ambalo limebeba kauli mbiu ya “Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya Uchumi” pia kutakuwa na matukio mengine muhimu ikiwemo kutamatisha wiki la vijana .

Mhe Ayoub amefafanua kuwa sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Amani pia zitakuwa ni mahsusi kwa ajili ya kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa Mwal Julius Kambarage Nyerere,ambapo zitaanza kwa ibada ya misa maalumu katika kanisa la Shangani Posta.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here