SHARE

Kiungo wa kati wa Manchester City Yaya Toure anasema kuwa kombe la dunia la mwaka ujao litakuwa na ”litafeli pakubwa iwapo litatawaliwa na ubaguzi wa rangi” .

Toure mwenye umri wa miaka 34 alikabiliwa na matamshi ya ubaguzi wa rangi wakati City ilipocheza dhidi ya CSKA Moscow katika kombe la vilabu bingwa nchini Urusi 2013.

Anataka kuisaidia Fifa na serikali ya Urusi kukabiliana na tatizo hilo kabla ya michuano hiyo kuanza rasmi.Lazima tuone mabadiliko kwa sababu hawalizungumzii swala hili na kuewa utatuzi, aliongezea.

Mwezi uliopita, Liverpool ililalamika kwa Uefa kuhusu madai ya matamshi ya ubaguzi wa rangi yaliomlenga winga Bobby Adekanye wakati wa mechi ya kombe la Uefa upande wa vijana katika uwanja wa Spartak Moscow.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here