SHARE

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Edinson Cavani kwa mujibu wa habari ameiomba Manchester City kumsajili.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mustakabali wake Parc de Princes umekuwa wa mashaka baada ya kuwa na mvutano dimbani baina yake na Neymar mwezi uliopita.

Edinson Cavani Neymar PSG Paris Saint-Germain

Katika kipidi cha pili cha mechi ambayo PSG walishinda 2-0 dhidi ya Lyon Septemba 17, Cavani na Neymar walikuwa wakigombea kupiga penalti, ambayo hata hivyo Cavani aliikosa.

Kwa mujibu wa Don Balon, mshambuliaji huyo wa zamani wa Napoli anaamini atakuwa tishio mbele ya goli kwa Man City na anaitegemea timu hiyo ya Guardiola kumsajili, lakini pia akiwa anazifikiria Real Madrid, Manchester United au Everton.

Madrid wanataka kusajili mshambuliaji mpya na wanayo machaguzi mengi, kadhalika Cavani atakuwa na wakati mgumu kumpokonya namba Romelu Lukaku Old Trafford.

Everton watahitaji nguvu nyingi kumshawishi Cavani kutua Goodison kutokana na kiwango chao duni cha sasa, wakiwa chini mkiani mwa msimamo wa ligi.

Hakuna taarifa zozote kama Manchester City wanafikiria kumsajili Cavani.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here