SHARE

Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini, TFDA, imezifutia usajili dawa mbalimbali za kutibu magonjwa ya binadamu na kuziondoa kwenye soko pamoja na kusitisha matumizi yake kutokana na kuwa na madhara makubwa kwa wagonjwa.

Hayo yamebainishwa Jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo, wakati akifungua mafunzo ya wakufunzi wa ufuatiliaji kuhusu ufundishaji na uhamasishaji wa masuala ya udhibiti wa madhara yatokanayo na matumizi ya dawa zisizo salama kwa watendaji wa afya kutoka Wilaya zote za mkoa wa Arusha.

Bw. Sillo amesema, katika kudhibiti matumizi ya dawa zisizofaa TFDA imeondoa dawa ya sindano aina ya Chloramphenical kwenye soko baada ya Shirika la Afya Duniani, WHO, kubaini dawa hiyo ina madhara kwa watumiaji, Pia mamlaka hiyo imefuta usajili wa dawa zingine kama vile Ketoconazole, pamoja na Celecoxib baada ya kuthibitika zina madhara kwa watumiaji.

Bw.Sillo amefafanua kwamba, lengo la mafunzo hayo ni kuongeza idadi ya wakufunzi wa masuala ya usalama wa dawa kutoka 73 hadi 133 na tayari katika kipindi cha miaka mitatu TFDA imehamasisha watendaji wa afya wapatao 2,000 kote nchini


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here