SHARE

Mamlaka ya Kuzuia na Kupamba na Madawa ya Kulevya (DCEA) nchini, imetoa ufafanuzi juu ya Marekebisho ya Sheria Namba 5 ya Mwaka 2017 ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya.

Katika mkutano wake na wanahabari, kwenye makao makuu ya mamlaka hiyo, Upanga jijini Dar, kamishna mkuu wa mamlaka hiyo, Rogers Siyanga amesema miongoni mwa vipengele vilivyorekebishwa ni kile cha wauza madawa ya kulevya ‘unga’ wakubwa kutupwa jela kifungo cha maisha huku wale wadogo wakikabiliwa na adhabu ya miaka 30 jela.

Amesema lengo la marekebisho hayo ya sheria yaliyofikiwa kwenye kikao cha bunge kilichopita, ni kuboresha utekelezaji wa sheria hiyo na kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu ya mamlaka kwa ufanisi na kuongeza kuwa vipengele vingine vilivyoboreshwa ni pamoja na kile kinachoipa mamlaka hiyo uwezo wa kupata taarifa kutoka vyanzo mbalimbali kama kwenye taasisi za serikali na kuwa na uwezo wa kutumia silaha pale inapobidi.

“Vingine vilivyorekebishwa ni pamoja na sheria kuongeza fursa kwa watumiaji wa madawa ya kulevya kupata matibabu na huduma nyingine badala ya kuhukumiwa kifungo gerezani.

“Pia sheria hii sasa itaiwezesha mamlaka kufanya uchunguzi wa sayansi jina, kuweka kifungu kitakachoruhusu kufanya mashauriani na taasisi au mamlaka nyingine za serikali, inampa uwezo Kamishna Jenerali kushikilia akaunti za benki za watuhumiwa wa madawa ya kulevya na kuzuia dhamana kwa makosa makubwa ya madawa ya kulevya yasiyostahili dhamana,” alisema.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here