SHARE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA leo ametembelewa Ofisini kwake na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania DETLEF WAECHTER na kufanya Mazungunzo.

Katika Mazungumzo hayo yalijikita kwenye Mikakati ya pamoja kwenye Maboresho ya Sekta za Afya, Elimu, Usalama na Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya.

Kuhusu Sekta ya Elimu Balozi huyo ameguswa na kampeni ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu kwenye Mkoa wa Dar es Salaam ambapo ameahidi kushirikiana na RC MAKONDA katika kampeni hiyo.

Aidha RC MAKONDA amewasilisha kwa Balozi huyo ombi la kujengwa kwa Jengo la huduma ya Dharura (ICU) kwenye Hospital za Mkoa wa Dar es salaam ambapo Balozi amelichukuwa ombi hilo kwaajili ya kulifanyia kazi.

RC MAKONDA amesema kuwa wamekubaliana kushirikiana katika mapambano ya Biashara ya Dawa za kulevya pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kulinda Jiji kwa kutumia Teknolojia.

Balozi wa Ujerumani Nchini Bwana DETLET WAECHTER amesema watashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika masuala yote ya Maendeleo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here