SHARE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Mhe. Uhuru Kenyatta kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili.

Taarifa ya serikali iliyotolewa leo na Mkurugenzi, Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi imethibitisha hilo.

Mhe. Kenyatta ataapishwa siku ya Jumanne, Novemba 28, 2017, jijini Nairobi, ikiwa ni baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here