SHARE

Magari 50 ambayo mwenyewe hajajulikana yamekamatwa bandarini na Rais Magufuli alipofanya ziara bandarini hapo, akitokea kwenye meli ya madaktari bingwa kutoka China.

Magari hayo amabyo yameelezwa kuletwa mwezi wa 6 mwaka 2015 yakiwa na magari ya jeshi la polisi, mpaka leo hayajatolewa bandarini hapo, yameelezwa kuwa na siri kuba ambayo Rais mwenyewe anaifahamu, huku mizgo wa lawama ukienda kwa Jeshi la Polisi.

‚ÄúInakuwaje rais nipate taarifa za magari kufichwa lakini Waziri, TRA, TPA msijuie? Mnatakiwa muwe na informer wenu sio hadi mimi nije ndo mnaaza kusema sijui. Nafahamu hata mletaji namfahamu, nataka mniletee ninyi ili nione kama tunaenda uelekeo mmoja au hatuendi”, amesema Rais Magufli.

Raius Magufuli ameendelea kwa kusema …”Kule Polisi kuna mambo ya hovyo. Polisi Mnadai hizi gari ni zenu, kwanini hamzifuatilii tangu 2015? Kuna magari yamekaa miaka 10 lakini sheria inasema gari likikaa zaidi ya siku 21 yapigwe Mnada, kwanini hampigi mnada? IGP kwenye Majambazi upo safi lakini huku kwenye Ufisadi bado sana. Kama mtu anakunanihii mtwange. Nilikuchagua ulikua such good guy lakini unaniangusha. Polisi kuna Uchafu mwingi sana”.

Kufuatia tukio hilo Rais Magufuli ametoa siku saba kwa TAKUKURU, Polisi na Wizara ya Uchukuzi kumpatia taarifa kamili juu ya magari hayio, ambayo mpaka sasa mmiliki wake hajajulikana.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here