SHARE

Msanii mkongwe na mtayarishaji wa muziki nchini, Dully Sykes amefunguka na kudai kuwa watayarushaji muziki wa Bongo fleva wa zamani walikuwa wakiingiza pesa nyingi  katika muziki kutokana na uchache wao tofauti na sasa

Dully amesema sasa hivi maproducer wamekuwa wengi kiasi kwamba hakuna tena biashara na kila mmoja anataka kumuiga mwenzake

“Maproducer wa zamani ni maproducer mamilionea lakini wa sasa hivi hawawezi kuwa mamilionea kwasababu maproducer wa sasa hivi wapo wengi sana na touch zao wana ‘mix sawa ndio maana unaona maproducer wengi wa zamani hawateteleki kila mmoja wana maisha. Maproducer wa zamani wapo vizuri walienda shule, wa sasa hivi si shule ni talent zao kwahiyo wanaambukizana talent  unakuta maproducer wamekuwa wengi kama sisi wanamuziki halafu wanaigana mwisho wa siku kunakuwa hakuna biashara” amesema Dully Sykes


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here