SHARE

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Ferooz ambaye anafanya vyema na wimbo wake ‘Nakaza roho’ ameweka wazi kuwa alichoimba kwenye wimbo huo ni ukweli mtupu na kusema kuna watu wake wa karibu kama Prof Jay, Chege wamempa kisogo.

Ferooz akipiga stori na mwandishi wa tovuti ya EATV amesema kuwa watu wake wa karibu wengi wao walimtenga na kumuweka pembeni na kudai hata alipojitahidi kuwatafuta lakini mawasiliano hayakuwa mazuri, jambo ambalo anasema hakutegemea kutokana na namna alivyokuwa akiishi na watu hao.

Mbali na hilo Ferooz anasema katika kipindi ambacho aliyumba kimaisha alizidi kukatisha tamaa na watu wengi mbalimbali lakini alijipa matumaini na kupigana jambo ambalo anaona limeanza kuleta matumaini kutokana na watu kumpokea vyema na wimbo wake huo mpya ‘Nakaza roho’

“Kiukweli namshukuru Mungu kwani wimbo huu umepokelewa vizuri na mashabiki wangu kila kona na sasa naanza kuona mtaani umeanza kufanya vizuri, kiukweli wimbo huu umenipa matumaini mapya kuwa naweza kufanya mambo makubwa kwani bado mashabiki wanapenda kazi zangu, sikutegemea kabisaa kama ningepeta mapokeo haya hivyo imenipa nguvu sana”alisema Ferooz.

Video ya Ferooz imeongozwa na director wa video anayechipukia nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Kilonzo. Itazame hapa zaidi


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here