SHARE

Dereva Bajaji, Maksood Khan, 28 kutoka nchini India amefanyiwa upasuaji wa tumbo na kutolewa fedha aina ya sarafu 263 ndani ya tumbo lake pamoja na misumari 100.

Novemba 19 mwaka huu, Khan, alifikishwa katika hospitali Sanjay Gandhi iliyopo nchini India baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa muda mrefu.

Madaktari wa hopsitali hiyo awali waliamini kwamba alikuwa amelishwa sumu na kuamua kumfanyia vipimo vya X-rays iliyoonyesha vitu vingi vilivyomo ndani ya tumbo lake.

“Alikuwa akilalamika kuwa na maumivu zaidi ya mwezi mmoja, ila baada ya uchunguzi tumegundua alikuwa na ugonjwa wa shinikizo la damu na alikuwa katika hali mbaya,” Amesema Dk Priyank Sharma.

“Tuligundua ndani ya tumbo kuna, minyororo, sarafu 263 na misumari karibu 100…Upasuaji ulichukua saa tatu kufanyika,” Dk. APS Gaharwal, mkuu wa idara ya upasuaji wa jumla, aliiambia CNN.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here