SHARE

Nilijibu kwa ujasili mkubwa. Mzee yule akanitaka kupumzika hukua akiahidi kuwa usiku wa siku hiyo tutafanya taratibu zote za kiapo kisha asubuhi ya kesho yake nitafanya safari ya kwenda Muifufu kukamilisha zoezi lililopo mbele yangu!..

Niliwatazama watu wale nikawaonea huruma sana, afya zao zilikuwa dhaifu na kumbe chanzo ni njaa ambayo imesababishwa na ukatili wa Magugi, niliingia ndani nikaenda kwenye chumba ambacho nilijikuta baada ya kuzinduka na kuchukua fuko lile kubwa ambalo lilikuwa na nyama bado na maji kidogo nikatoka na kuwapati watoto wadogo ambao nilikuwa nawaona pale wakiwa na afya isiyo ya kuridhisha “hawa wananyonya, hawali chakula” nilishangazwa na kauli ile ambayo ilitoka kwa  mwanamke mmojawapo pale kwa maana umri wao ulitosheleza kuwa wameanza kula “huku kwetu mtoto hunyonya mpaka hapo maziwa yatakapoisha kwa mama yake, chakula tunachopata huwa hakitoshi hivyo ni bora ale mama ili aweze kumnyonyesha mtoto, wote wapate” alifafanua yule mzee nikasikitishwa sana na ugumu wa maisha ya watu wale. Nikamkabidhi mwanamke yule mzigo ule ili yeye apange matumizi mazuri kwa maana niligundua kuwa pamoja na udogo wake kilikuwa na maana kubwa kwa watu wale…

Nikabaki nikiongea hili na lile na mzee yule huku akinithimulia mambo mengi ya zamani na jinsi ambavyo anayatamani tena maisha ya  dunia ya kawaida ambayo yalikuwa mazuri na mepesi sana hata anajutia kuwa kwake mchani na hatimaye kuangukia Muifufu…
“lakini mzee mimi ninavyoelewa ni kuwa watu wote ambao walikimbia dunia ya kawaida na kujificha Muifufu hawakuweza kuzaliana tena, mbona huku mna watoto?” niliuliza swali na mzee akanijibu “watu wa Muifufu pia wanaweza kuwa na maisha tofauti kama watengwa kama ambavyo tulitengwa sisi, laana ya kutozaliana tuliipata kwa umoja ule, kwakuwa sisi sio sehemu yao tena, laana ile haituhusu tena” alifafanua mzee yule, nikamuelewa na kuendelea na habari nyingine mpaka kiza kilipoingia ambapo watu walianza kukusanyika kwenye uwanja wa nyumba ile na kulipotulia nikaitwa na kukalishwa kwenye kiti ambacho kilikuwepo katikati ya watu wale wakiwa wamekizunguka na kufanya mduara, mzee yule akaja na kuanza kusema maneno huku akinitaka kumfuatisha “mimi Abubakar Saire, ninaahidi kutekeleza makubaliano ambayo tumewekeana na kama nisipotekeleza basi kiapo hichi kiishi na mimi mpaka kitakaponitoa uhai wangu” yalisemwa maneno hayo huku nikifuatisha mpaka tukamaliza kisha akazunguka nyuma yangu na kunichanja na kitu chenye ncha kali mgongoni, hayakuwa maumivu makali kama ambavyo nilitegemea, na hapo kazi ikawa imemalizika. Watu wale wakaanza kuondoka huku kila mmoja wao akipita mbele yangu na kunipa mkono huku wakitoa maneno ya kunitakia mafanikio.

Asubuhi siku iliyofuata nikaongea na mzee yule na kumuuliza juu ya utekelezaji wa kazi ambayo wao walipaswa kuifanya.. “kila kitu kitakuwa sawa wakati unaingia Muifufu wewe kuwa tayari kwa safari” alisema mzee yule na safari ya kurudi Muifufu ikawa tayari, nikaondoka kijijini pale nikisindikizwa na wakazi wa kijiji kile mpaka mlimani kisha wakarudi na kuniacha nikipanda mlima ule…

usikose sehemu ya 38


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here