SHARE

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu mpya ya msanii Issa Musa ‘Cloud 112’ kesho Jumamosi (Desemba 2) ndani ya Ukumbi wa Cinemax, Mlimani City jijini Dar.
Akifanyiwa mahojiano mafupi na mtandao huu mchana huu, Cloud 112 aliyewahi pia kutamba na filamu kibao ikiwemo Toba na Tripple L alisema kuwa, Waziri Mwakyembe atakuwepo katika uzinduzi huo utakaoanza saa moja za usiku kumuwakilisha Makamu wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
“Utakuwa uzinduzi wa aina yake kutokana na aina ya filamu yenyewe. Ujue Filamu ya Usijisahau kwa asilimia 95 imechezewa nchini Sweden na asilimia 5 hapa Bongo hivyo nimekuja kuwaonesha ladha ya filamu iliyopotea kwa muda mrefu.
“Tunatarajia kuizindua kwa kishindo kwanza Mlimani City chini ya mgeni rasmi Waziri Mwakyembe na baada ya hapo atatuzindulia tena Zanzibar pale Ngome Kongwe, Desemba 8. Uzinduzi huu utaendelea tena kwa wakazi wa Tanga katika Ukumbi wa Majestic, Desemba 9 hivyo niwaombe wapenzi wote wa filamu kujitokeza kwa wingi kushuhudia uzinduzi huu wa kihistoria,” alisema Cloud 112.
Filamu ya Usijisahau imetayarishiwa nchini Sweden chini ya kampuni yao ya Aismu Entertainment ambapo imeongozwa na muongozaji Fabian kutoka nchini Sweden.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here