SHARE

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga na watani zao wa jadi Simba kwa mara ya kwanza watausaka ubingwa wa Kombe la Kagame nchini Djibout mwakani.

Djibout imepewa wenyeji huo katika kikao Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), kilichofanyika leo jijini Nairobi na kutaja nchi zitakazokuwa wenyeji wa mashindano mbalimbali yatakayofanyika mwakani.

Tangu Rais wa Rwanda, Paul Kagame awe mdhamini wa mashindano hayo hii ni mara ya kwanza kufanyika Djibout nchi ambayo klabu zake hazina rekodi ya kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Katika mashindano Tanzania bara itawakilishwa na Yanga bingwa mara tano wakati Simba amenyakuwa taji hilo mara sita wataingia kwa lengo la kuendeleza rekodi yao nzuri katika kombe hilo.

Simba mara ya mwisho kuchukua ubingwa wa mashindano hayo ilikuwa 2002, wakati Yanga ilitwaa ubingwa huo mara mbili mfululizi katika fainali zilizofanyika Dar es Salaam 2011 na 2012.

Mabingwa watetezi Azam itashiriki fainali za mwakani kutetea taji lake ililochukua 2015, kwa kuifunga Gor Mahia mabao 2-0 kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam.

Baada ya Azam kunyakuwa ubingwa mashindano hayo hayakufanyika tena kutokana na changamoto za kukosa udhamini na nchi wanachama wa Cecafa kutokuwa tayari kuandaa mashindano hayo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here