SHARE

Nilipoamka giza lilikuwa limeingia tayari, nikatoka nnje na kumkuta mmoja wa vijana wale akiwa busy kukusanya kuni kutoka huko mashambani na kuleta pale nyumbani “bwana, mbona Sauda hakuja? unajua sio salama mimi kuendelea kuwepo hapa bila muongozo wake” nilimsemesha bwana yule ambaye alikuja mpaka pale nilipokuwa nimesimama akanitaka kukaa chini naye akakaa kisha mazungumzo yakaanza “bwana kuna jambo unapaswa kulifahamu juu ya bi.Sauda” alianza kuelezea bwana yule na moyo wangu ukapiga paaah!, nikiona dalili ya kuwepo kwa habari mbaya kutokana na utulivu aliouonesha bwana yule kwenye kunipatia habari hizo..

“Nini kimetokea?” niliuliza na bwana yule akaanza kunielezea “mpaka wakati huu tunaoongea bi. Sauda amekamatwa na bwana Magugi na hukumu yake inategemewa kutolewa kesho” alielezea kijana yule nikapatwa na mshituko mkubwa sana, sikutegemea jambo lile kutokea kabisa, Sauda ndiye aliyekuwa kiongozi wa mipango yote, kukamatwa kwake nilikuona kama kukwama kwa kila kitu. “ilikuwaje mpaka akakamatwa?” niliuliza na kijana yule akatoa maelezo “wapelelezi wa Magugi wamekuwa wakimfuatilia mwenendo wake na kugundua kuwa amekuwa akitoka nyumbani kwake mara kwa mara hata usiku mwingi hivyo wakamfikishia taarifa hizo Magugi ambaye alipata mashaka juu yake na kuamuru akamatwe.

Tulipotoka kukusindikiza wewe tukakuta habari za kukamatwa kwake na bwana Magugi ameahidi kutoa hukumu kesho baada ya kujua ukweli juu ya mwenendo wa Sauda” alimaliza kuelezea kijana yule, nikafikiria kwa muda kisha kumuuliza tena kijana yule “unadhani Magugi ataweza kuugundua ukweli?” kijana yule akanijibu “yani baada ya kukamatwa kwake tu sisi tulikata tamaa ya kuwanaye tena, Magugi akiutaka ukweli huwa haukosi” nikatulia na kufikiria kwa muda kisha kumuuliza tena kijana yule.. “kwanini ninyi mmejitolea kumfuata Sauda hata kumsaliti Magugi ikiwa mnajua hatari iliyopo ikiwa mtakamatwa?”…

“Ni kwakuwa sisi tunaujua ukweli ambao watu wengi wa Muifufu hawaujui, ukweli ambao tumeupata kwa msaada wa Sauda na kuamua kuanzisha harakati za chinichini za kuwakomboa watu wote” alijieleza vizuri, lakini nilikuwa na maswali mengine ya kumuuliza.. “ni watu wangapi ambao mmejitolea kuwepo upande wetu mpaka sasa?” niliuliza, naye akanijibu “siijui idadi kamili lakini tuko wengiwengi kidogo, Sauda amekuwa akihakikisha tunakuwa na mtu kila sehemu, amekuwa pia akichagua wananchi ambao anawaona wanaweza kufaa iwapo wataujua ukweli na kuanza nao taratibu mwisho kuwarudishia kumbukumbu ambazo Magugi alizifuta vichani mwao, na kujaribu kuwaondoa hofu ambayo wamekuwa wakiishi nayo juu ya Magugi ambapo baadhi hufanikiwa ila ambao hawafanikiwi hua wanauwawa kwa maana wanakuwa wamepata siri ambazo wanaweza kuzitoa na kusababisha matatizo” alimaliza kunielezea nami nikauliza “je hakuna mtu wa karibu kidogo na Magugi ambaye yuko upande wetu?” kijana yule akanijibu “hapana ingawa Sauda aliwahi kumshawishi mshauri mkuu wa Magugi ambaye ni Mjomba wake lakini alikataa na mipango ya kumuua haikufanikiwa lakini hakuwahi kusema chochote, nadhani kwakuwa alikuwa karibu sana na Mnaro na alimpenda sana”

Alielezea kijana yule na moja kwa moja nikapata hamu ya kutaka kuonana na mtu huyo “nawezaje kuonana na huyo mjomba wake?” kijana yule akanielezea “labda umfuate kwake kwa maana huwa sio mtu wa kutoka sana” alinielezea kijana yule nami nikamtaka anipeleke kwa huyo mtu naye akawa tayari.
Tukaenda mpaka kwenye nyumba moja kubwa ambayo haikuwa mbali sana na pale tulipokuwepo, tukakaribishwa na mwanamke wa makamo ambaye nilitambulishwa kuwa alikuwa mtoto wa mzee ambae tulikwenda kumuona pale “mmh! mzee amelala tayari” alielezea mwanamke yule baada ya kuambiwa kuwa tulikuwepo pale kwaajili ya kuonana na baba yake..

“Ni suala la haraka sanaa, tunaomba utuamshie” nilieleze lakini mwanamke yule alionekana kutaka kupinga, lakini aliponyanyua kinywa chake tu kutaka kuongea mimi nikamuwahi “tafadhali tusaidie, ni jambo la uhai au kifo” nilisema huku nikimkazia macho nikiamini udhaifu wa wanawake utanifaa na kweli, hakuongeza neno zaidi ya kuelelea kumuamsha baba yake!…


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here