SHARE

Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali za Chalenji vijana chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwakani.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao Baraza la vyama vya soka la Afrika Mashariki na Kati CECAFA, kilichofanyika leo jijini Nairobi.

Uamuzi huo wa Cecafa umekuja wakati Tanzania ikiwa katika harakati za maandalizi ya fainali za vijana za Mataifa ya Afrika AFCON 2019.

Mbali ya kuipa wenyeji Tanzania, pia kikao hicho kimetangaza Uganda kuwa mwenyeji wa mashindano ya soka la ufukweni na Kombe la Chalenji kwa wanawake mwakani, wakati Kenya au Sudan wakitaraji kuwa wenyeji wa Chalenji kwa Vijana chini ya miaka 20 mwakani.

Hata hivyo, Cecafa imeshindwa kufikia uamuzi ni nchi gani itakuwa mwenyeji wa fainali za mwakani za Kombe la Chalenji ya mwaka.

Katika hatua nyingine Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Cecafa kwa miaka miwili ijayo.

Awali kinyanganyiro hicho kiliwavutia wanachama wanane kabla ya watatu kujiondoa na hivyo watano hao kuchaguliwa bila kupingwa.

Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Petra Dorris Kenya.

Wajumbe hao wataungana na Rais wa kamati hiyo Mutasim Gafar wa Sudan watakuwa na kazi ya kuboresha utenda kazi wa baraza hilo kwa ajili ya kuimarisha soka ukanda huo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here